Monday, March 12, 2012

Kilio cha Watanzania Nchini Ugiriki

Kaka Michuzi Habari za maisha na Maendeleo,Nilikua naulizia hivi ni Kweli Serikari ya Tanzania inasaidia Raia wake kurudi Nyumbani kutoka Ugiriki?

Kwa kuwa vijana wengi tumeamua kurudi nyumbani kutokana maisha yamekuwa magumu sana na pia tunashindwa hata nauri ya kurudia,tumeshajiandikisha kurudi kwa hiari lakini bado majina yetu kuitwa kutokana kuna zaidi ya watu milioni pia wa mataifa mbali mbali wamejiandikisha ikiwemo Afganistani wao ndio wanaongoza.

Kibaya zaidi imekua hata pa kulala tunashindwa kulipa hizo euro tano tano kwa mwezi kwa kuwa imebidi tukae nyumba watu labda 7 hadi kumi,na nyumba zenyewe kupatikana imekua tabu Chakula tabu.

Nyumba hazina hata umeme,madeni ni makubwa.
Hata wagiriki wenyewe wanasikitika,kula ukipata mara moja tu ushukuru kwa siku.

Na kutoka hapa kuelekea ulaya nyengine gharama zake ni mara mbili ya kutoka Bongo kuja Ulaya kwa kuwa connection ya rahishi angalau kufika Italy tu ni 2500 ukipata chini ya hapo basi ni passport feki unakamatwa unakua ushapoteza hela.

Imebidi baadhi yetu kuna ambao wamejipatisha vitanda hospitalini ili kuweza angalau kupata sehemu ya kuweka ubavu na chakula,huku Omonia kuna foleni chakula cha bure lakini hadi ukiifikia kishamalizika.

Je ni kweli kuna utaratibu unaofanywa na serikali ya Tanzania kutusaidia kurudi?
Maana tulipita hapa kutafuta maisha lakini hao ndugu zetu wa zamani hapa bichi wao wanasikitika na wengi wanarudi kwa vile wamekua na akiba ila sisi ndio tunaofika hapa tunapata shida ni balaa tupu na pia wametushauri tuondoke ijapokua baadhi wanatusaidia saidia.

Ahsante

Mdau wa Ugiriki

No comments:

Post a Comment