Mashabiki wa timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam,wakiwa wamefurika kwa wingi ndani ya uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuishangilia timu yao inayoingia dimbani muda mfupi ujao kumenyana na timu ya Kiyovu ya nchini Rwanda katika mashindano ya Kombe la Shirikisho ikiwa ni mchezo wa pili mara baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa awali huko nchini Rwanda.
Baadhi ya Wanahabari wakiwapiga picha watu waliokuwa wamevalia kinyago cha mfano wa mnyama Simba.
Wachezaji wa Simba wakipiga jalamba kabla ya mchezo kuanza.
Wachezaji wa Kiyovu ya nchini Rwanda wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mchezo.
Globu ya Jamii inakuwa bega kwa bena na Wewe Mdau kuhakikisha inakuletea kina kinachojiri uwanjani hapa na pia Mchezo huu unatangaza Live kupitia Radio Clouds Fm
hivyo BOFYA HAPA kusikiliza.
No comments:
Post a Comment