Siku za hivi karibuni kumejitokeza tabia si ya uanamichezo kwa baadhi ya mashabiki wa soka kurushiana viti uwanjani pale Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Naomba hili niliweke sawa kama mchango wangu kwa taasisi husika,ili iwe changamoto na pengine suluhisho la tatizo zima.Nadhani baadhi ya mashabiki mtakubaliana na mimi kabisa kwamba pale uwanjani kuna idadi ya viti vingi sana havina NATI za kushikia yaani viti viko loose.
NINI CHANZO?
Kwa macho yangu niliwahi kushuhudia kwenye mechi moja kijana mmoja akiwa na kiroba kimejaa CLAMPS (Clamp ni chuma kinachoshikilia kiti kwa chini kisha kinafungwa kwa nati.) Nilichofanya niliripoti kwa askari yule kijana akakamatwa na alipoulizwa alisema anaenda kuuza vyuma chakavu.
Hata hivyo,pamoja na hayo sikubaliana na upuuzi unaofanywa na baadhi ya mashabiki kurusha viti.Lakini kwa upande mwingine hoja ya kwamba viti vinang’olewa mimi siafikiani nayo kabisa.Vile viti vimefungwa kwa uimara mkubwa sana, hakuna mtu anaweza kung’oa kwa kutingisha tu,lazima kwanza awe na spana kisha ainame chini kufungua kiti (Inahitaji time).
Nini maana yake sasa? Ni kwamba,vile viti vinavyorushwa uwanjani mashabiki wanavikuta vikiwa havijafungwa yaani viko loose na ndipo matatizo yanapoanzia.
MAONI YANGU!
Wenye mamlaka na usimamizi wa Uwanja wa Taifa wachukue hatua za maksudi kufanya ukaguzi na kurudishia nati katika viti vyote.Pili,uwepo usimamizi wa kutosha na hasa kwa watoto wadogo ambao wanakua na viroba uwanjani kwa kisingizio cha kuokota chupa kumbe wanafungua nati.Na tatu,tuwe na ulinzi shirikishi kwa kila mtu pale uwanjani kuwa mlinzi wa mwenzake kwa kutangaza motisha ya pesa taslimu kwa mtoa habari yeyote (Kama manispaa ya mji wa Moshi inavyofanya) juu ya uharibifu wa mali kuanzia viti,switch,taa,koki,na wanaokojolea katika masinki ya maji.
Huu ni mtazamo wangu,
Furaha “Mkatakona”
No comments:
Post a Comment