Wednesday, March 14, 2012

angalizo la globu ya jamii: Leteni picha na habari za siasa zichapishwe

Kumekuwa na uhaba wa picha na habari kutoka vyama vya siasa, ukiondoa CHADEMA na CCM, kiasi hata inaonekana kuna kutoa kipaumbele kwa vyama hivyo tu. Hii bila shaka inasababishwa na changamoto za maofisa uhusiano/habari wa vyama vingine, ambao hawachangamkii ipaswavyo fursa hii isiyo gharama ya kutangaza vyama na shughuli zao. Yaani ukiona picha na habari za chama fulani zinashamiri humu ujue kuwa maafisa habari wake wanachangamkia fursa hii bila ajizi na si vinginevyo.

Globu ya Jamii inasimamia kwa dhati sera yake ya HATUBAGUI, HATUCHAGUI; ATAYETUZIKA HATUMJUI. Hivyo shime vyama vya siasa amkeni na mlete habari zenu zichapishwe bila malipo, sharti likiwa mradi usichafue hali ya hewa ama usijeruhi hisia za mtu/watu.

Lete habari zenu tuzichapishe  bila malipo kupitia
issamichuzi@gmail.com




No comments:

Post a Comment