WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka (shoto) na Mada Maugo leo Wametambulisha rasmi mkanda huo ambao utashindaniwa Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju alisema kuanikwa kwa mkanda huo kutaashiria kupamba moto kwa ambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.
"Tunauanika mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda," alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D.
Thursday, March 22, 2012
Waziri Mkuu na Balozi wa Korea Kusini nchini wazindua chuo cha VETA cha mkoa wa Pwani
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Balozi wa Korea Kusini nchini, Bw. Young Hoon Kim wakikata utepe kuashiria kuzindua chuo cha VETA cha mkoa wa Pwani kwenye eneo la Kongowe Machi 21, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Tanzia
Marehemu Emmanuel Luther Nsunza ( 1951 -2012)
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA –TRL, MHANDISI KIPALLO AMANI KISAMFU ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA NDUGU EMMANUEL LUTHER NSUNZA MHASIBU MKUU MSAIDIZI WA TRL, KILICHOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA TUMAINI –DAR ES SALAAM SIKU YA JUMATANO MACHI 21, 2012
MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU CHANG’OMBE JUU KWENYE NYUMBA ZILIZOKUWA ZA TRC.
HESHIMA ZA MWISHO ZITATOLEWA NYUMBANI KWA MAREHEMU SIKU YA IJUMAA MACHI 23 , 2012 KUANZIA SAA 3 ASUBUHI NA ATASAFIRISHWA KWENDA SINGIDA SIKU YA JUMAMOSI MACHI 24, 2012.
HABARI ZIWAFIKIE :
- Wazazi wa Marehemu EMMANUEL LUTHER NSUNZA WALIOKO SINGIDA
- NDUGU LINFORD NOAH MBOMA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA –TRC NA VIONGOZI WOTE WA LILILOKUWA SHIRIKA LA RELI TANZANIA –TRC
- MWENYEKITI WA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA RELI TANZANIA –TRAWU
- WAFANYAKAZI WOTE WA KAMPUNI YA TRL NA WALE WALIOKUWA KATIKA TRC
- NA PAMOJA NA NDUGU , JAMAA, JIRANI NA MARAFIKI WA MAREHEMU
BWANA AMETOA , BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE..!
WAUZA MBOLEA FEKI WAKAMATWA SONGEA
Wafanyabishara wa mbolea waliokamatwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma jana kwa tuhuma za kuuza chumvi walioiweka katika mifuko ya mbolea na kuwauzia wananchi kama mbolea aina ya SA, kutoka kushoto Abdilai Abdala(42) Yasin Gawaza(48) Festo Sanga(25) na Ajda Halfan(36) wakiwa katika kituo kikuu cha polisi mjini songea.
PICHA NA MUHIDIN AMRI.
PICHA NA MUHIDIN AMRI.
SHUKURANI TOKA VICTORIA FOUNDATION KWA WAFADHILI
Mwenyekiti wa Victoria Foundation Bi Vicky Kamata akitoa msaada wa vyakula,maziwa,matunda,mavazi na magodoro kwa watoto Yatima FTI Masumbwe.
MHESHIWA VICKY KAMATA MBUNGE WA GEITA VITI MAALUM NA MWENYEKITI WA VICTORIA FOUNDATION ANAPENDA KUTOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA MAKAMPUNI , TAASISI NA WATU BINAFSI WALIOJITOA KWA HALI NA MALI KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WALEMAVU MKOA WA GEITA, MWENYEZI MUNGU AWARUDISHIE MARA MIA KWA MOYO WAO WA UPENDO.
WATU NA TAASISI HIZO NI PAMOJA NA EWURA, HOME SHOPPING CENTRE, QUALITY GROUP LIMITED, TRA, GEITA GOLD MINE, MHESHIMIWA MARK BOMANI, PPF, UDF (UNITY IN DIVERSITY FOUNDATION), MKURUGENZI HALIMASHAURI YA WILAYA GEITA NA MERY NOTMAN (KIDSCARE IRELAND)
Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi yafunguliwa leo jijini Dar
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(kushoto) akipongezwa na Mbunge wa Jimbo la Peramio, Jenister Mhagama mara baada ya kufungua , Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam.
Baadhi ya Wabunge walioshiriki Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa mara baada ya kufungua , Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam.Picha zote na MAGRETH KINABO - MAELEZO
Subscribe to:
Posts (Atom)