Thursday, March 22, 2012

KUFUNGWA KWA MASHINDANO YA UCHORAJI NA KUTOA ZAWADI

Siku ya Jumamosi tarehe 24/03/2012 kutakuwa na kufungwa na kugawa zawadi kwa washindi wa Mashindano ya Uchoraji yaliyobeba kichwa cha Habari cha Miaka 50 ya Taifa yakishindanisha Tasisii za Elimu kuanzia shule za awali ,Msingi,Sekondari na Vyuo ,mashindano yaliyoandaliwa na Image Profession.

Hafla ambayo itatanguliwa na maonyesho ya picha za washiriki wa shindano pamoja na kuonyesha picha za wachoraji wazoefu kuanzia saa 11 :00 (Saa Tano)asubuhimpaka saa 14 :00(Saa Nane)Mchana kwenye Ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya Taifa makabala na Chuo cha Fedha(I.F.M.)

Njoo ushuhudie Vipaji katika Sanaa za Uchoraji ,njoo uwape moyo Washiriki na pia uweze kujifunza mambo mengi yahusuyo sanaa hii ya uchoraji.
Pia Njoo ujuwe kichwa cha habari cha Mashindano ya Mwaka huu 2012.

WENU KATIKA UJENZI WA SANAA NA MICHEZO
Image Profession & iP Sports Club

kitabu kipya cha simulizi kiko mitaani


JINA LA KITABU: MALIPO NI HAPAHAPA
      MTUNZI:  ADELA DALLY KAVISHE 
Adela Daly Kavishe (pichani)   ni mtangazaji wa radio passion FM ambayo inarusha matangazo yake jijini Dar es salaam Ninayofuraha kukamilisha kitabu cha simulizi cha MALIPO NI HAPAHAPA ambacho kimebeba simulizi tatu za kusisimua ikiwemo simulizi inayoitwa DADA YANGU,MAMA MDOGO pamoja na simulizi iliyobeba jina la kitabu MALIPO NI HAPAHAPA 
 Kitabu cha Malipo ni Hapahapa na simulizi nyingine za maisha kinaonyesha hali halisi ya maisha tunayoishi, matatizo tunayokutana nayo na namna ya kutatua matatizo tunayoyapata kwa wakati huo. Pia kwa kusoma kitabu hiki utajifunza mengi kwani kinatoa  picha halisi ya maisha yetu ya kila siku.
Ndani ya kitabu hiki nimezungumzia maisha na mapenzi katika mtazamo halisi na pia kinaonyesha namna mapenzi yanavyoweza kuyageuza maisha kuwa machungu na mafupi. 
Ukianza kusoma kitabu hiki hutakiacha hadi ukimalize kwani hadithi zilizomo zimesheheni matukio ya kusisimua ambayo moja kwa moja yanalenga maisha yetu ya kila siku.
Kupitia vitabu vya simulizi za maisha kama vile kitabu hiki, tunajifunza mambo mengi ambayo yanatusaidia kuishi katika mazingira tofauti ikiwa ni katika shida au raha na hata kujua namna ya kuishi na watu wanaotuzunguka.
Utapata kitabu hiki kwa  bei ya sh 5000 tu.
 Kwa mawasiliano kuhusu upatikanaji wa kitabu hiki.
Tafadhali tumia no zifuatazo +255652343430 au +255752817444
Au kavisheadela@yahoo.com  Unaweza pia kuingia humu http://www.adeladallykavishe.blogspot.com 

bomoa bomoa kupisha kituo kikuu cha mabasi yaendayo kasi kuzikumba nyumba za shirika la reli na bandari gerezani jijini dar alfajiri ya leo

 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Meck Sadick akiongea na waandishi wa habari jioni ya leo juu ya bomoa bomoa ya nyumba za mtaa wa Gerezani zilizokuwa zinamilikiwa na shirika la Reli pamoja na mamlaka ya bandari. Zoezi hilo litafanyika kuanzia kesho saa kumi na moja alfajiri, pia amewataka wakazi wanaoishi maeneo hayo wawe wameishahama katika maeneo hayo kabla zoezi hilo kufanyika. Amesema zoezi hilo litafanywa na kampuni ya Yono action mart ili kupisha ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo kasi.

Wawakilishi kutoka wakala wa serikali (DART)pamoja na (YONO ACTION MART)wa kwanza kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa (DART) Bw.Cosmas Takule. Katikati  ni Mkurugenzi mtendaji wa Yono Bi Scholastica Kevela na kulia Afisa masoko Yono action mart Bw. Joseph Assey. 
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON)

rais kikwete afunga maonesho ya maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani iringa leo

 Mto Ruaha ukionekana kutoka juu ukitiririsha maji ambao Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuchukua hatua madhubuti za kuunusuru mto huo dhidi ya uharibifu ili kuleta tija zaidi katika kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji umeme.Rais Kikwete ametoa ahadi hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji iliyofanyika kitaifa Mkoani Iringa .
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kilichofanyika kitaifa katika uwanja wa Michezo wa Samora mkoani Iringa
 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia bustani ya mfano inayotumia utaalamu wa kumwagilia kwa matone(drip Iririgation) wakati wa maonyesho yaliyofanyika katika Uwanja wa michezoi wa Samora mkoani Iringa
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi ya kutibu maji kutoka kwa mtaalamu wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho katika uwanja wa michezo wa Samora mjini Iringa. Picha na Freddy Maro 
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Maji Vijijini Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Amani Mafuru wakati akitoa taarifa ya wiki ya maji mkoani Irinaga leo, Kushoto ni Naibu Waziri wa maji Mh. Grayson Rwenge.
 Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa maji Mijini Wizara ya Maji na Umwagiliani Bw.Yohana Monjesa katika kilele cha wiki ya maji mkoani Iringa.
Mtaalam wa Maendeleo ya Jamii katika mradi wa wa Mazingira katika Ziwa Victoria BwRaymond Mariki akitoa maelezo ya utekelezaji wa majukumu ya mradi huo mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika maonyesho ya wiki ya maji Mkoani Iringa yaliyomalizika leo.

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu na na wafadhili (mstari wa mbele) sambamba na kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya maji Kitaifa yalifikia tamati leo na kufungwa rasmi na Rais Kikwete mapema leo jioni kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Rais Jakaya Kikwete akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na Kupokelewa na Mkurugenzi wake wa Mahusiano na Mawasiliano Teddy Mapunda. Pia SBL walipokea Cheti cha ushiriki wa maonesho hayo. 
 Baadhi ya viongozi  wa Serikali na wageni waalikwa wakiwa ameketi jukwaa kuu
Rais Kikwete akielekea kukagua Mabanda ya maonesho ndani ya Uwanja wa Samora mapema jioni hii,ambapo Rais Jakaya Kikwete leo amefunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa Mkoani Iringa. Pamoja na kuhutubia katika kilele hicho pia Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya watoa huduma za maji na wadau mbalimbali wa maji nchini.
Pichani ni Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Bi Teddy Mapunda mara baada ya kulitembelea banda hilo,ambao ndio wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo ya mwaka huu yaliyofanyika uwanja wa Samora Mjini Iringa. na pichani kati ni Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Bi Teddy Mapunda akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni rasmi,Mh Rais Kikwete  mara baada ya kulitembelea banda hilo.

Mh. Lowassa akuatana na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto,Monduli leo kujadili hali ya elimu ya shule hiyo

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza kwa kusisitiza wakati wa mkutano wake na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto,Wilayani Monduli kuhusiana na hali ya elimu katika shule hiyo kutoridhisha na kupelekea wanafunzi wengi wa shule hiyo kufeli kwenye mtihani wa taifa wa kidato cha nne.Mkutano huo umefanyika leo shuleni hapo,ambapo walimu wa shule hiyo walitoa changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo.Mh. Lowassa amewaasa walimu wa Shule hiyo kuwa wafanye kazi kwa juhudi ili kuwaandaa vijana wa taifa la baadae.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Bw. Joseph Lukumay.
Afisa Elimu Wilaya ya Monduli,Bw. Shaaban Mngunye (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) wakati wa mkutano na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto,Wilayani Monduli.Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo,Mwl. Ally Muyago na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Bw. Joseph Lukumay.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Shule ya Sekondari ya Engutoto,Bw. Joseph Lukumay akitoa maelezo mafupi na kuwataka walimu wa shule hiyo kuanza kuzungumzia ni kwanini shule yao imefanya vibaya kwenye mtihani wa taifa wa kidato cha nne.
Mwalimu wa Shule ya Shule ya Sekondari ya Engutoto iliyopo Wilayani Monduli Mkoani Arusha akitoa taarifa fupi ya shule kwa Mh. Edward Lowassa ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo la Monduli,wakati wa mkutano wake na Walimu wa Shule hiyo kuhusiana na hali ya elimu katika shule hiyo kutoridhisha na kupelekea wanafunzi wengi wa shule hiyo kufeli kwenye mtihani wa taifa wa kidato cha nne.
Walimu wa Shule ya Engutoto iliyopo Wilayani Monduli Mkoani Arusha,wakizungumzia changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo katika kazi yao ambapo wengi wamedai kuwa inachangia kwa kiasi fulani kudhorota kwa elimu katika shule hiyo.

NIHILENT announces strategic partnership designed to mutually benefit local companies scale up and grow their business.

Mr Minoo Dastur, Chief operating officer and Director of  Nihilent (centre) speaks to reporters today at the Holiday Inn in Dar es salaam today. Right is Mr   Ravi Teja, Vice President of Global Consulting  and right is Mr  Davie Kahwa the  Chief Executive O fficer of Equip. 

NIHILENT, aleading global consulting and solutions intergration Company and EQUIP GRC, an advisory firm that provides governance, risk management and internal audit transformation solution, today announced a strategic partnership designed to mutually benefit both companies to scale up and grow their business.

This strategic partnership will address the requirement for local capability builiding around sound business management practices, especially in the area of Business and information Technology consulting. This partnership is a direct response to the pro- investment and pro-growth policies and " New Vigor, New Zeal, and New speed" theme pursued diligently by the progressive government which seeks to unleash Tanzania's talent growth potential. 



While Equip brigs with it leading practices in corporate governance, risk management, regulatory compliance and internal audit transformation , Nihilent brigs hard rigor and  plentiful experience into effective deployment through its competence around corporate strategy execution capability. 


Equip and  Nihilent will combine their expertise to address the business challenges facing organizations in the Financial Services, Government and state-run enterprises and Supply chain and Logistics. 

BODI YA TASAF WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA PEMBA

 Mkuu wa mkoa wa pemba Mh Juma kassim Tindwa ( katikati mwenye suti nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja  na  ujumbe wa bodi ya Mfuko wa maendeleo ya jamii ulio chini ya ofisi ya Rais (TASAF) ulipomtembelea ofisini kwake nakumfahamisha kazi wanayo ifanya kisiwani hapo
Bi Hadiya Mwinyi Suedi akipiga ngoma huku akiongoza kikundi cha Msondo  kuburudisha  ujumbe wa bodi ya TASAF  pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo walipofika katika kisiwa cha Pemba kwa ajili ya kukagua miradi inayo dhaminiwa na TASAF  

CHEKA VS MAUGO WAONESHWA MKANDA WA UBINGWA LEO

WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka (shoto)  na Mada Maugo leo Wametambulisha rasmi mkanda huo ambao utashindaniwa Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju alisema kuanikwa kwa mkanda huo kutaashiria kupamba moto kwa ambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

"Tunauanika mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda," alisema Kaike.

Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.

Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.

Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.


Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D. 

Waziri Mkuu na Balozi wa Korea Kusini nchini wazindua chuo cha VETA cha mkoa wa Pwani

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Balozi wa Korea Kusini nchini, Bw. Young Hoon Kim wakikata utepe kuashiria kuzindua chuo cha VETA cha mkoa wa Pwani kwenye eneo la Kongowe Machi 21, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tanzia

Marehemu Emmanuel Luther Nsunza ( 1951 -2012)

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA –TRL, MHANDISI KIPALLO AMANI KISAMFU ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA NDUGU EMMANUEL LUTHER NSUNZA MHASIBU MKUU MSAIDIZI WA TRL, KILICHOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA TUMAINI –DAR ES SALAAM SIKU YA JUMATANO MACHI 21, 2012

MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU CHANG’OMBE JUU KWENYE NYUMBA ZILIZOKUWA ZA TRC.

HESHIMA ZA MWISHO ZITATOLEWA NYUMBANI KWA MAREHEMU SIKU YA IJUMAA MACHI 23 , 2012 KUANZIA SAA 3 ASUBUHI NA ATASAFIRISHWA KWENDA SINGIDA SIKU YA JUMAMOSI MACHI 24, 2012.

HABARI ZIWAFIKIE :
  • Wazazi wa Marehemu EMMANUEL LUTHER NSUNZA WALIOKO SINGIDA
  • NDUGU LINFORD NOAH MBOMA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA –TRC NA VIONGOZI WOTE WA LILILOKUWA SHIRIKA LA RELI TANZANIA –TRC
  •  MWENYEKITI WA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA RELI TANZANIA –TRAWU
  •  WAFANYAKAZI WOTE WA KAMPUNI YA TRL NA WALE WALIOKUWA KATIKA TRC
  • NA PAMOJA NA NDUGU , JAMAA, JIRANI NA MARAFIKI WA MAREHEMU

BWANA AMETOA , BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE..!

WAUZA MBOLEA FEKI WAKAMATWA SONGEA

Wafanyabishara wa mbolea waliokamatwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma jana kwa tuhuma za kuuza  chumvi walioiweka katika mifuko ya mbolea na kuwauzia wananchi kama mbolea aina ya SA, kutoka kushoto Abdilai Abdala(42) Yasin Gawaza(48) Festo Sanga(25) na Ajda Halfan(36) wakiwa katika kituo kikuu cha polisi mjini songea.
PICHA NA MUHIDIN AMRI.

SHUKURANI TOKA VICTORIA FOUNDATION KWA WAFADHILI

 Mwenyekiti wa Victoria Foundation Bi Vicky Kamata akitoa msaada wa vyakula,maziwa,matunda,mavazi na magodoro kwa watoto Yatima FTI Masumbwe.



MHESHIWA VICKY KAMATA MBUNGE WA GEITA VITI MAALUM NA MWENYEKITI WA VICTORIA FOUNDATION ANAPENDA KUTOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA MAKAMPUNI , TAASISI NA WATU BINAFSI WALIOJITOA KWA HALI NA MALI KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WALEMAVU MKOA WA GEITA, MWENYEZI MUNGU AWARUDISHIE MARA MIA KWA MOYO WAO WA UPENDO. 

WATU NA TAASISI HIZO NI PAMOJA NA EWURA, HOME SHOPPING CENTRE, QUALITY GROUP LIMITED, TRA, GEITA GOLD MINE, MHESHIMIWA MARK BOMANI, PPF, UDF (UNITY IN DIVERSITY FOUNDATION), MKURUGENZI HALIMASHAURI YA WILAYA GEITA NA MERY NOTMAN (KIDSCARE IRELAND)

Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi yafunguliwa leo jijini Dar

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(kushoto) akipongezwa na Mbunge wa Jimbo la Peramio, Jenister Mhagama mara baada ya kufungua , Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam.
 Baadhi ya Wabunge walioshiriki Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa mara baada ya kufungua , Semina Elimishi ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi katika hoteli ya White Sands jijini Dares Salaam.Picha zote na MAGRETH KINABO - MAELEZO

news alert: Tido Mhando awa Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication Limited

Pichani Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Profesa Palamagamba Kabudi akimkaribisha ofisini Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MCL Tido Mhando, katikati ni Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo Theophil Makunga. Picha na Mwananchi




Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,Inaeleza kuwa Boss wa zamani wa TBC (Tanzania Broadcasting),Tido Mhando (pichani) amekuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya kila siku hapa nchini ya Mwananchi Communication Limited,kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani wa Kampuni hiyo,Sam Shollei.

Globu ya Jamii inatoa pongezi kwa Bw. Tido Mhando kwa kupata nafasi hiyo na kumtakia kila la kheri katika utendaji wa kazi yake hiyo mpya.

Rais Dk. Shein katika sherehe za CCM Wilaya wa Magharibi Zanzibar

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai,wakati wa sherehe za uwekaji wa Jiwe la msingi la Maskani ya Ari Mpya,kasi Mpya na Nguvu Mpya huko kijiji cha Kama Bondeni Wilaya ya Magharibi leo,katika ziara maalum ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akimkabidhi kadi ya CCM,UWT Riziki Khamis Abdalla,akiwa ni miongoni mwa wanachama waliokabidhiwa kadi za CCM,baada ya kujiunga na chama hicho,wakati wa sherehe za uwekaji wa Jiwe la msingi la Maskani ya Ari Mpya,kasi Mpya na Nguvu Mpya huko kijiji cha Kama Bondeni Wilaya ya Magharibi leo,katika ziara maalum ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi.
Msoma Utenzi katika sherehe za Uwekaji wa jiwe la msingi Maskani ya Ari Mpya ,Kasi Mpya na Mpya,Farida Rajab,akihani utenzi wake uliotoa burudani ndani yake,baada ya Mjumbne wa Kamati Kuu ya CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein,kuweka jiwe la msingi Maskani hiyo huko Kijiji cha Kama Bondeni leo akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Magharibi.
Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi CCM,wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za Chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,wakati wa sherehe za uwekaji wa Jiwe la msingi la Maskani ya Ari Mpya,kasi Mpya na Nguvu Mpya huko kijiji cha Kama Bondeni Wilaya ya Magharibi leo,katika ziara maalum ya kuimarisha
Chama cha Mapinduzi.Picha na Ramadhan Othman Ikulu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI
WA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA KAGERA (KRFA).
 TAREHE 21/03/2012
 
1.                   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawajulisha wadau wa soka kwamba uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Kagera ulifanyika tarehe 17 Machi 2012, Bukoba mjini kama ulivyokuwa umepangwa. Uchaguzi huo ulifanyika kwa mujibu wa Katiba ya KRFA na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF.
 
2.                   Viongozi waliochaguliwa kwenye Kamati ya Utendaji ya KRFA ni hawa wafuatao:
 
(i)                   Mwenyekiti:                                                 Ndg. Jamal E. Malinzi
(ii)                 Makamu Mwenyekiti:                                   Ndg. Alex Raphael Gashaza
(iii)                Katibu Mkuu:                                               Ndg. Salum H. Umande
(iv)               Mweka Hazina:                                           Ndg. Adolf Martin Mahuguli
(v)                 Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF:                   Ndg. Peregrinius A. Rutayuga
(vi)               Mjumbe- Mwakilishi wa Vilabu:                     Ndg. Didas David Zimbihile
(vii)              Wajumbe- Kamati ya Utendaji:          -           Ndg. Abubakari Kazinja
-           Ndg. Dionise Magezi
-           Ndg. Ezekiel Geofrey Samson
 
3.                   TFF inawashukuru wadau wa soka Mkoani Kagera, hususan, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KRFA na Kamati ya Uchaguzi ya KRFA kwa kuheshimu na kuzingatia Katiba ya KRFA,  Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, hivyo kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi wa KRFA kama ulivyopangwa. Ni matumaini ya TFF kuwa wadau wa soka Mkoani Kagera wataendelea kushirikiana na TFF kuendeleza soka katika Mkoa wa Kagera.
 
Sunday Kayuni
KAIMU KATIBU MKUU

Askari Polisi Ajishindia Milioni 10 za M-PESA

Mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza hayupo pichani. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(kushoto)akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo.Katikati ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(kushoto)akimsikiliza Mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo(kulia)Baada ya kukabidhiwa rasmi  mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 na Mkurugenzi huyo,Katikati ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya Mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo,kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza hayupo pichani,Jumla ya Milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wapili toka kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani,wakati wa kumkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo watatu.kulia ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox,kushoto Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Biashara Mwamvita Makamba. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari wakifatilia makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 kwa mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo.aliyokabidhiwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.Jumla ya Milion 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
 
========  ====== =======

Askari Polisi Ajishindia Milioni 10 za M-PESA

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imemkabidhi hundi mshindi wa zawadi ya kitita cha Shilingi Milioni Kumi wa droo ya mwezi ya promosheni ya M-PESA Bw Peter James Kilalo.

Bw. Kilalo amekabidhiwa hundi hiyo leo jijini Dra es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacoim Tanzania Bw. Rene Meza katika hafla fupi iliyohudhuriwa pia na waandishi wa habari.

Akipokea hundi yake Bw. Kilalo ambae ni Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Dar es salaam ameshukuru kw akuibuka mshindi jambo ambalo amesema hakulitegemea.

"Kwa kweli mimi ni mteja mzuri sana wa M-PESA lakini kweli sikutegemea kwamba ningeibuka mshindi, ila sasa ninapopokea hundi hii naamini kwamba nimeshinda na fedha hizi Milioni kumi ni zangu"Alibainisha Bw. Kilalo.

Alipoulizwa namna alivyojipanga kutumia pesa hizo Bw Kialalo alijibu" Jamani mimi ni masikini na sikuwahi kuota kwamba ipo siku nitashinda kiasi kikubwa cha fedha namna hii hivyo jambo kubwa kwangu kwa wakati huu ni kwanza kuacha akili yangu itulie kabisa ndio niamue niziwekeze wapi ili zinikwamue kimaisha"Alisema

"Nina mawazo kadhaa ya biashara ambayo nimekuwa nikiyawaza kama njia ya kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha hivyo hizi pesa nitazielekeza huko ila baada ya akili yangu kwanza kutulia kutoka katika hali ya furaha niliyonayo sasa."Aliongeza

Mshindi huyo ametumia pia fursa hiyo kuwashauri watanzania kutumia huduma ya M-PESA kwa kuwa mbali na kwamba imerahisisha maisha katika utumaji na upokeaji fedha mijini na vijijini bado wanaweza kuwa katika nafasi ya kushinda kama yeye

Awali  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema promosheni hiyo imelenga kuwawezesha wateja wa M-PESA kubadili masiha kutokana na wanavyotumia huduma hiyo.

"Promosheni hii tulizindua mwezi uliopita tukilenga kuwawezesha wateja wetu kujishindia zawadi za fedha taslimu, kiasi cha Shilingi Milioni 480 kinashindaniwa ambapo hadi sasa wateja zaidi ya 4,000 wameshajinyakulia zaidi ya Shilingi Milioni 120" Alisema Bw. Rene

AmesemaVodacom inatambua umuhimu wa huduma ya M-PESA katika maisha ya kila siku ya wananchi na hivyo wakati wote imekuwepo mikakati imara ya kuiwezesha huduma hiyo kuendelea kuwa bora zaidi,salama na ya kuaminika sokoni.

"Matumizi ya huduma ya M-PESA hapa nchini yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana, kiwango cha wananchi kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo ya bidhaa mbalimbali kupitia M-PESA ni kikubwa jambo ambalo linakuwa rahisi zaidi kutokana na mtandao mpana tulionao wa mawakala wanaofikia 20,000 mijini na vijijini." Aliongeza Bw Rene

Promosheni hiyo itadumu kwa siku tisini kutoka Februari 13, 2012 hadi May 13, 2012. Mbali na kutoa mshindi mmoja wa shilingi milioni kumi kila mwezi pia kila siku washindi mia moja hujishindia Shilingi 50,000 kila mmoja.